Kampuni ya ALAF Tanzania imezindua rasmi Tuzo ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka wa 2025, ambapo wanaotarajiwa kushiriki shindano hilo wametakiwa kuwasilisha kazi zao kwa ajili ya kupitiwa na majaji.Hii ni tuzo ya 10 tangu kuanzishwa kwake 2015 na inafadhiliwa na kampuni ya ALAF.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na swala hilo, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa ALAF Limited Tanzania, Hawa Bayumi alisema tuzo hiyo inaendelea kukua huku ikivutia washiriki wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

























