SIKU chache baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kumteua Rashid Mwinyishehe (Kingwedu) kwenda kuwania ubunge katika Jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam,www.diramakini.co.tz imebaini kuwa, ameunda kikosi kazi imara cha kampeni ambacho kimepanga kutwaa jimbo hilo ambalo kwa muda limekuwa chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) likiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu.
![]() |
| Picha na Mtandao |
"Mimi nimezaliwa Kisarawe, lakini Ilala pia ni nyumbani kwa baba yangu, nimeamua kugombea hapa Ilala kwa sababu ninaijua vizuri, nimeona nisimpe presha mdogo wangu Selemani Jafo, na kusema kweli kwanza simuwezi,"Kingwendu.
Tovuti hii imebaini kuwa, kikosi cha ushindi kitaongozwa na Meneja Kampeni wake ambaye ni Bambo (Dickson Samson Makwaya) huku Meneja Msaidizi akiwa ni Mtanga Mtangalile, endelea kufuatilia www.diramakini.co.tz tutakujuza zaidi...
