TRA yaja na Kampeni ya Elimu ya Kodi ya Mlango kwa Mlango, RC Andengenye ataja faida zake, atoa wito kwa wafanyabiashara

MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema amefurahishwa na Kampeni ya Elimu ya Kodi ya Mlango kwa Mlango inayoendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Kigoma huku akiwatoa hofu wafanyabiashara wanaohofia kunyang’anywa faida zao badala yake wanatakiwa kutumia nafasi hiyo kuhoji maswali na kupata elimu.

Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akitoa elimu ya kodi kwa mfanyabiashara wa eneo la Sokoni mkoani Kigoma leo.

RC Andengenye ameyasema hayo baada ya kutembelewa na maafisa wa TRA kutoka makao makuu waliofika mkoani hapa kwa ajili ya kuendesha kampeni hiyo ya elimu ya kodi mlango kwa mlango.

Amesema, huu ni wakati wa wafanyabiashara wa kukidhi kiu yao ya maswali kuhusu kodi pamoja na changamoto wanazokutana nazo ili waweze kutatuliwa na maofisa hao wa TRA ambao wamekuja kukusanya fedha za Serikali zinazotokana na biashara wanazofanya.

Amesema, kampeni hiyo itawawezesha kujua kuwa pesa zinazokusanywa sio za TRA na kwamba ni za Serikali ambazo zitamgusa kila mmoja kutokana na miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na Serikali.

Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akitoa elimu ya kodi kwa mfanyabiashara wa eneo la Sokoni mkoani Kigoma leo.

“Nawashauri wafanyabiashara watoe ushirikiano kwa maofisa wetu na sehemu ambayo watakuwa hawajaelewa wanatakiwa kuuliza ili kuelekezwa, huu ni wakati wao na lengo ni kujenga urafiki baina ya TRA na walipakodi,”amesema Andengenye.

Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Kigoma, Jackob Mtemang’ombe amesema kuwa , mkakati wa TRA ni kuhakikisha inaeneza elimu ya kodi kwa kila mwananchi kwa urahisi na kwamba kampeni hiyo ya mlango kwa mlango ni nzuri kutokana na kuwa elimu itawafikia kwa urahisi kutokana na kuwa watafikiwa katika maeneo yao.

Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakipata baraka za kutoa elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango  toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Thobias Andengenye leo.

Amesema ni vingumu kwa walipakodi kuacha biashara zao na kuhudhuria semina za kodi, hivyo TRA imeamua kuwuafata ili kuwarahisishia ikiwa ni pamoja na kuona mazingira wanayofanyia biashara zao na changamoto wanazokutana nazo.

“Ni rahisi kumuelimisha mlipakodi akiwa katika eneo lake la biashara ukilinganisha akiwa mbali na baada ya kuwaelimisha ndipo tutaanza kufuata sheria, kwani watakuwa wameshapata uelewa,”amesema Mtemang’ombe.

  Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news