Amasha Sumaye anasa kwenye mtego wa makachero

AMASHA Sumaye (49) ambaye ni dereva  na mkazi wa Ngaramtoni mkoani Arusha anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Manyara kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu tisa wakiwemo wanawake watano na wanaume wanne.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Paul Kasabago amethibitisha tukio hilo.

Amesema, Septemba 7, 2020 majira ya saa tatu asubuhi huko katika kituo cha Polisi Minjingu Kata ya Nkaiti Wilaya ya Babati askari walifanya upekuzi wa magari katika Barabara Kuu ya Arusha-Babati ndipo walipomkamata mtuhumiwa huyo.

Pia Kamanda huyo amewataja wahamiaji hao haramu kwa upande wa wanawake amesema ni Sahra Bashiri, Halima Abdi, Ubah  Abdukadir,Mulk Ramadhani,Samia Ramadhani na kwa upande wa wanaume ni Abdrazack mohamed, Abdi Mohamed,  Farah Duban na Isse Abdkadir wote wakiwa ni raia wa Somalia.

Amefafanua kuwa, wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa kwa njia haramu ya kuvunja sheria za nchi, kutoka Arusha kuelekea mpakani mwa Tanzania na Zambia  ambapo mbinu iliyotumika ni kuwaficha kwenye gari  na kuwasafirisha, gari lililotumika kuwasafirisha ni T.797 DFW aina ya Toyota Noah.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Paul Kasabago amesema,chanzo cha uhalifu  huo ni kujipatia kipato kwa njia haramu, "watuhumiwa wote 10 wapo katika kituo cha Polisi Babati kwa uchunguzi zaidi,"ameieleza www.diramakini.co.tz


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news