Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuchia huru mfanyabiashara Jennifer Jovin (Niffer) na Mika baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuondoa mashtaka dhidi yake.
Uamuzi huo umetolewa Desemba 3, 2025, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamuya, kufuatia kuwasilishwa kwa hati ya Nolle Prosequi taarifa rasmi ya DPP ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka kwa mujibu wa kifungu cha 92(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, marejeo ya 2023.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
























