SHIRIKA lisilo la Kiserikali linalojiusisha na mambo ya utafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii (SSSRC) limesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeoneshwa kupendwa zaidi na wananchi kutokana na uchapakazi wa Rais Dkt.John Magufuli.
Hatua hiyo imetokana na utafiti uliofanywa na shirika hilo kupitia njia ya dodoso na mahojiano ambapo zaidi ya watu 1876 walifikiwa kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa matokeo ya utafiti wa mwenendo wa uchaguzi mkuu nchini, Mkurugenzi wa SSSRC, Maximillian Makori amesema, utafiti huo ulijikita katika vyama vya siasa ikiwemo ACT Wazalendo, CUF, CHADEMA, pamoja na CCM.
Amesema, katika utafiti huo, mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameshika nafasi ya pili kwa asilimia 14.7, mgombea wa ACT-Wazalendo, Bernad Membe asilimia tatu, na mgombea wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipata asilimia moja, huku vyama vingine vikipata asilimia 0.5.
Maximilian amesema miogoni mwa sababu zilizotajwa kwa wigi wananchi kumuunga mkono Rais Dkt John Magufuli ni namna anavyochapa kazi katika kuboresha miundombinu, kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma pamoja na mapambano ya rushwa.
Kwa upande wa mgombea wa CHADEMA, utafiti huo umeonyesha wananchi kumkubali Lissu kwa asilimia 14 kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja, na kumuonea huruma.
“Utafiti huu tumetumia njia ya mahojiano na madodoso, upande wa Zanzibar tuliwafikia watu 1,316 na kwa bara 560 ujumla tumetekeleza utafiti huu katika mikoa 27.
“Kwa kutumia mahojiano ya ana kwa ana tuliwafikia watu 480 kwa Tanzania bara na kwa kutumia dodoso tuliwafikia 612, kwa njia ya simu 224, kwa upande wa Zanzibar mahojiano ya ana kwa ana tulifanya kwa watu 321, 239 kwa mahojiano ya ana kwa ana,”amesema.
Maximilian amesema vijana wenye umri wa miaka 18-40 walionyesha kuikubali CCM kwa asilimia 43, CHADEMA asilimia 42, ACT Wazalendo asilimia 10 na vyama vingine asilimia tano.
“Upande wa maeneo Rais Dkt.Magufuli anakubalika zaidi kwa asilimia 83 vijijini, na mijini kwa asilimia 73.1 huku mgombea wa CHADEMA, vijijini akikubalika kwa asilimia 13 na mijini asilimia 20 na wagombea wa vyama vingine wakikubalika kwa asilimia 1-3 kwa vijijini na asilimia 1-4 kwa mijini,”amesema.
Kwa upande wake Mtafiti Mwandamizi wa SSSCR, Peter Kasela alisema, utafiti huo pia ulionyesha Rais Dkt. Magufuli anakubalika zaidi na wanawake kwa asilimia 79.9 na wanaume asilimia 58 huku Lissu akikubalika kwa asilimia 34 kwa wanaume na asilimia 17 kwa wanawake.
ACT-Wazalendo asilimia tatu kwa wanawake na asilimia saba kwa wanaume na wengine ni asilimia moja ambapo kwa upande wa utafiti wa majimbo wataanza kutoa kila wiki.Endelea kusoma hapa.
Dokta Magufuli awabwaga Lissu, Lipumba, Membe
Tags
Siasa