Maalim Seif: Mkinipa ridhaa nitazifanyia maboresho sheria, kuwezesha uhuru wa kusafiri duniani, vitambulisho vya uraia, hati

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali yake itaheshimiu utu na ubinadamu kwa ustawi wa Zanzibar, anaripoti Talib Ussi (Diramakini) Zanzibar.

Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais Zanzibar kupitia ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad (hayupo pichani). (Diramakini).

Ameyasema hayo Septemba 30, 2020 huko Mapofu Wingwi katika mkutano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake za kuomba kura kwa wananchi visiwani Zanzibar.

Amesema, iwapo wananchi wanampa ridhaa atahakikisha Serikali yake inalinda haki za binadamu ili kila mmoja aishi bila hofu wala kuteswa na atakuwa huru kufanya analolitaka ilimradi asivunje sheria. Pia Maalim Seif amesema kuwa, mtu yeyote atakuwa huru kutoa mawazo yake pamoja na vyombo vya habari kufanyakazi bila kuingiliwa.

Mgombea Urais Zanzibar kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharrif Hamad akiwahutubia wananchi Septemba 30,2020 katika eneo la Mapofu Wingi. (Diramakini).

Maalim Seif amesema, sheria zote ambazo zinaonekana kikwazo kwa wananchi iwapo atapewa ridhaa na wananchi atahakikisha anazifuta au kuzifanyia maboresho ili ziendane na wakati. Sambamba na hilo Maalim Seif amesema, haki nyingine ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanakuwa huru kuishi na kwenda watakako bila kubugudhiwa na kufahamisha kuwa atahakikisha paspoti ni haki ya kila mwananchi.

Kwa upande mwingine amesema, mtoto akizaliwa atapewa namba yake pale pale na kueleza namba hiyo ndio itakayotumiwa kwa kupatiwa paspoti pamoja na leseni. Maalim Seif amesema, atahakikisha wananchi wake wote wanapewa vitambulisho cha urai wa Zanzibar na kila cha mkaazi watapatiwa wageni tu.

Kwa upande wa kuabudu, Maalim Seif ameeleza kuwa, Serikali yake itatoa uhuru wa kuabudu kwa kila mwananchi kufuata dini anayoitaka na wakati anaoutaka. Amesema, atahakikisha Seriikali haimtesi mtu wala kumuonea kwa sababu tu ya kuabudu bali itaheshimu kwa sababu ni haki yake ya msingi.

Wakati huo huo, Maalim Seif amemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Saimon Sirro kumuondoa katika nafasi yake OCD wa Wilaya ya Micheweni kwa madai kuwa anatumika kisiasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news