Haya ndiyo mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu aliyofunguka kuelekea Oktoba 28

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu huku akirejea kuwa, haijawahi kutokea uchaguzi ukawa rahisi, "lakini huu ni mgumu zaidi ikizingatia hali ya upatikanaji fedha;
Ameyasema hayo leo Septemba 9, 2020 wakati akizungumza na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam.

"Hatujidanganyi kwamba kazi ni nyepesi, kwani kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa kweli kweli, mimi nimeshiriki chaguzi tangu mwaka 1995 na kati ya hizo mbili nilishinda, nafahamu uchaguzi wa Tanzania ulivyo mgumu kwa chama chochote cha upinzani,"amesema.

Mbali na hayo Lissu amesema, wamemaliza awamu ya kwanza ya kampeni za Uchaguzi Mkuu katika kanda 10 za chama hicho huku uzoefu wao katika kanda ukionesha kwamba, wananchi wana kiu kubwa ya uwepo wa mabadiliko ya kisiasa nchini.

“Kesho tunaanza kampeni awamu ya pili baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya uzinduzi kwa kanda 10, tumeona matamanio ya Watanzania, wanataka mabadiliko na tumeona nguvu yetu,”amesema. Tundu Lissu pia tutakuwa na kituo chetu cha kukusanyia matokeo, hakuna sheria inayokataza kukusanya matokeo kutoka kwa mawakala.

“Tunataka Tume ya Uchaguzi ichapishe fomu za kutosha, sheria inataka kila wakala apewe nakala ya matokeo,"amesema huku akiongeza kuwa,suala hilo litapunguza mgogoro kati ya Tume ya Uchaguzi, vyama vya siasa na mawakala nchini.

Wakati huo huo, CHADEMA kimesema sasa wanakiunga mkono Chama cha ACT Wazalendo kwa upande wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu 2020.

"Hii inatokana na historia ya Zanzibar kuwa na wanachama wengi wa CCM na ACT -Wazalendo," amebainisha mgombea urais huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news