Maalim Seif asema akichaguliwa wote watapewa mikopo ya biashara, wasio na uwezo wa kuoa au kuolewa Serikali itawarahisishia

Mgombea Urais Zanzibar kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atatoa mikopo kwa wafanyabiashara ili waweze kukuza bishara zao na kutimiza malengo yao ya kuwa na familia bora, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ameyaeleza hayo katika Viwanja vya Mkele Jimbo la Shauri Moyo Wilaya ya Mjini Magharibi jijini Zanzibar wakati akiendelea kunadi ilani ya chama hicho na kuomba kura kwa wananchi visiwani humo.

Amesema kuwa, wafanyabiashara ni kundi muhimu katika nchi kwa hiyo katika Serikali yake atawaangalia vyema na yeyote anayetaka kuwekeza au kufanya biashara basi watakuwa na nafasi ya kupata mkopo na kurudisha wenyewe kwa taratibu.

“Kuna wafanyabishara wengine wanakuwa na biashara zao,lakini kutokana na mtaji mdogo zinakufa, lakini katika Serikali ambayo nitaiongoza nitahakikisha mitaji imenyanyuka,"amesema Maalim Seif ambaye ni pia ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa.

Kwa upande wa wananchi wake ambao wana mawazo mazuri ya kuwekeza, lakini hawana mitaji mgombea huyo amesema ataweka taratibu nzuri za mikopo ili waweze kupata chanzo cha kuwekeza na baadae waweze kutoa ajira kwa vijana.

“Tukifungua kampuni pamoja na viwanda ni msaada mkubwa kwa Serikali, kwani wananchi wetu watapata ajira humo humo,”amesema.

Amesema, nchi nyingi ambazo zimetumia utaratibu huo zimekuwa na wananchi walioajiriwa kwa asilimia kubwa.

Ameeleza kuwa, anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya biashara hivyo ni lazima aweke mipango madhubuti ya kufikia hatua hiyo.
Leo asubuhi Maalim Seif alifanya ziara ya kutembelea masoko ambapo alifika soko la Mikunguni na kuzungumza na wafanyabiashara sehemu hiyo.

Amesema, anasikitika viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wanasema uchumi umepanda wakati wananchi wana shida nyingi mpaka biashara zao zimekufa.

“Lakini sisi tutazifufua biashara zenu kwa kukupatieni mikopo,"amesema.

Kwa upande mwingine,Maalim Seif amesema baada kutoa mikopo hiyo atahakikisha ajira zinazotolewa kuanzia Serikalini hadi katika makampuni hakuna ubaguzi.

Sambamba na hilo amesema, ataweka utaratibu bora wa kutoa ajira kwa vijana ili wale ambao hawana uwezo wa kuoa na wao waweze kuoa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news