Maalim Seif asema akipewa ridhaa wakulima wa viungo, wafugaji watapiga hatua kiuchumi

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema endapo atapata ridhaa za Wazanzibar kuongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar atahakikisha wakulima wa viungo na karafuu wanakuwa huru kuuza mazao yao sehemu yoyote wanayotaka duniani, anaripoti TALIB USSI (Diramakini) ZANZIBAR.

Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad akipokea trei za mayayi mara baada ya kutembelea eneo la ufugaji linalomilikiwa na Humud Mohammed Said katika Kijiji cha Mtambile Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni sehemu yake ya kampeni kisiwani Pemba. (DIRAMAKINI).

Maalim Seif ameyaeleza hayo katika Kijiji cha Konde Wilaya ya Micheweni ikiwa ni muendelezo wa kampeni kupitia chama hicho katika Kisiwa cha Pemba.

Amesema, kazi ya Serikali yake itakuwa ni kukusanya kodi ndogo ili kuwafanya wakulima wapate faida kubwa ili waweze kuendeleza kazi yao hiyo kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

“Katika Serikali ya CCM imekuwa ikichukuwa faida kubwa kulikoni wakulima wenyewe, lakini Serikali ambayo nitaiongoza nitahakikisha inachukuwa kodi ndogo na kuwafanyia mazingira ya kukuza kilimo chao,"ameeleza Maalim Seif.

Amesema, kazi kubwa ya Serikali yake ni kuwapatia mbinu na mazinggira ya wakulima wa karafuu pamoja na bidhaa za viungo (spicies) nyingine ili iwe ni njia ya kukuza uchumi Wazanzibar.

“Tunataka kuwalea wakulima wetu wa bidhaa za viungo ili waweze kuitangaza Zanzibar katika masoko ya Ulimwengu ili baadae wafanyabisha za vingo waje Zanzibar kununua wenyewe,”amesema Maalim Seif.

Amesema, katika Serikali ya Chama Cha Mapinduzi wakulima wa bidhaa za viungo wanaonekana kuchoka sana kutokana na kuandamwa na kodi kubwa za kila sehemu.

Sambamba na hilo Maalim Seif amesema, katika utawala wake atawashauri wakulima wa bidhaa za viungo kujikita zaidi kwenye bidhaa za viungo ambavyo vitaleta tija za haraka kwao na Serikali kwa ujumla.

Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad akipokea kuku aliyopewa mara baada ya kutembelea eneo la ufugaji linalomilikiwa na Humud Mohammed Said katika Kijiji cha Mtambile Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni sehemu yake ya kampeni kisiwani Pemba. (DIRAMAKINI).

Pia Maalim Seif ambaye ni Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa amesema, kazi nyingine ya kufanya ni kuhakikisha Zanzibar inakuwa mifugo bora na soko la uhakika.

Amesema, atahakikisha huduma zote za mifugo zinapatika ili kile kinachozalishwa kiweze kuwa bora kwa mahitaji ya masoko yote.

“Tutahakikisha viwanda vya madawa ya vyakula na vya mifugo yote vinapatikana hapa hapa kwetu ili iwe rahisi wafugaji kuhudumia mifugo yao,"ameeleza Maalim Seif.

Amesema, wafugaji wengi wa kuku visiwani Zanzibar wameacha kufanya kazi hiyo kutokana na upatikanaji na gharama za madawa na vyakula visiwani Zanzibar.

Akizungumza mbele ya mgombea huyo, mfugaji wa kuku katika Kijiji cha Mtambile Mkoa wa Kusini Pemba, Humud Muhammed Said amesema, kama ingekuwa chakula cha kuku kinatengenezwa Zanzibar hata tija ingeongezeka.

Amesema, kwa mfano kwa siku yeye anahitaji matumizi ya magunia mawili na nusu kwa siku ambalo moja ni shilingi 55,000.

“Angalia kwa mwezi nitahitaji ngapi kwa maana hiyo hatuwezi kupata faida nzuri kutokana na ughali wa vyakula na kama yangalikuwa yanazalishwa Zanzibar bei hiyo haiwezi kufikia huko,”amesema Said.

Pia amesema, mbali na vyakula kuna madawa ambayo nayo wanagizia nje ambayo mara nyingine yanachelewa sana na kueleza wakati mwingine yanaweza kufika huku mifugo ikiwa imechelewa kupatiwa.

Kufuatia malalamiko hayo, Maalim Seif amesema katika utawala wake atafanya mapinduzi katika sekta ya mifugo na kilimo cha viungo na karafuu kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news