TAMWA Zanzibar yawajengea uwezo wajasiriamali kuzalisha kwa faida

IMEELEZWA kuwa, uboreshwaji wa bidhaa zitokanazo na wajasiriamali visiwani Zanzibar ni miongoni mwa njia muhimu zitakazowawezesha wajasiriamali visiwani hapa kuweza kuongeza soko la bidhaa zao kitaifa na kimataifa, anaripoti TALIB USSI (Diramakini) ZANZIBAR.

Mkufunzi wa ubora wa bidha za wajasriamali kutoka Taasisi ya Mboga na mMtunda, Sanje Lufwelo akiendelea na zoezi la ufundishaji kwa wajasiriamali walioshiriki mafunzo ya siku moja yalioandaliwa na TAMWA-Zanzibar. (DIRAMAKINI).

Kauli hio imetolewa na Afisa Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kutoka TAMWA-Zanzibar, Nairat Abdalla Ally kufuatia mafunzo maalumu ya siku moja yenye lengo la kuwajengea uwezo wajasiriamali hao katika uboreshaji wa vifungashio kwenye bidhaa zao mbalimbali. 

Amesema, mafunzo hayo yamewashirikisha wajasiriamali 30 kutoka shehia 12 za Unguja kwa lengo la kuwakomboa wanawake katika dimbwi la umaskini na kuondokana na utegemezi kwenye familia zao.

Amesema, kwa miaka mingi Zanzibar wapo wajasiriamali ambao wameamka na wenye kujishughulisha na kazi mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa, lakini wamekua wakikabiliana na chnagamoto za hapa na pale hususani ubora wa bidhaa zao jambo ambalo alisema wanahitaji kusaidiwa.

‘’Tunaamini kuwa mafunzo haya ya vifungashio kwa wajasiriamali hawa 30 yataleta tija na kufungua milango zaidi ya kibiashara ndani na nje ya nchi,’’amesema.


Baadhi ya wajasiriamali kutoka maeneo tofauti ya Unguja walioshiriki mafunzo ya siku moja yalioandaliwa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA)-Zanzibar yenye lengo la kuwawezesha wajasiriamali hao kuboresha bidhaa zao kwa kutumia vifungashio vyenye ubora.(DIRAMAKINI).

Sambamba na hayo Afisa huyo ametoa wito kwa wajasiriamali walionufaika na mafunzo hayo ya siku moja kuhakikisha wanayafanyia kazi ipasavyo ili yaweze kuleta tija kwao na familia zao.

Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Taasisi ya Mboga na Matunda, Sanje Lufwelo amesema utolewaji wa amfunzo ya vifungashio kwa wajasiriamali ni jambo muhimu kwa wakati huu ambao kuna ushindani mkubwa wa bidhaa za wajasiriamali.

Ameeleza kuwa, ili bidhaa iwe bora inahitaji mpangilio hususani kwenye muonekano kabla ya kuanza kwa matumizi ya bidhaa hizo kwa wateja.

‘’Kikawaida mteja huvutiwa na muonekano kabla ya kupata ladha ya kilichomo ndani, hivyo unapofeli kwenye kuweka bidhaa zako katika kifungashio bora ni wazi kuwa utawakosa wateja na kushindwa kupiga hatua katika maendeleo,’’ameongezea.

Baadhi ya wajasiriamali hao wamesema, wana matumaini makubwa na mafunzo hayo na kwamba watayafanyia kazi ipasavyo ili waweze kupata tija.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news