Mahakama ya Jumuiya Afrika Mashariki imetupilia mbali madai ya kupinga uhalali wa Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofunguliwa na baadhi ya wanaharakati nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
![]() |
| Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata akizungumza na vyombo vya habari. (Diramakini). |
Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata ameyasema hayo Septemba 30,2020 huku akifafanua kuwa, Mahakama hiyo imetoa uamuzi huo baada ya kukubaliana na hoja zote za upande wa Serikali.
Miongoni mwa hoja ni pamoja na madai kuletwa nje ya muda, pamoja na uhalali wa Mahakama kuhoji uhalali wa Muungano huo.
Wakili Mlata anasema, Mahakama ya Afrika Mashariki imezaliwa kupitia makubaliano ya The East African Community Treaty ya mwaka 1999 na kuanza kufanya kazi mwaka 200, hivyo Mahakama hiyo haina mamlaka ya kuhoji Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964.
