NRA yaja na Ilani jumuishi, shirikishi kwa Watanzania wote,Mahona ataja vipaumbele baada ya Oktoba 28

CHAMA cha National Reconstruction Alliance (NRA) kimezindua rasmi ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ambayo inatoa mwanga na muongozo bora juu ya namna ambavyo baada ya Watanzania kuwapa ridhaa ya uongozi Oktoba 28, mwaka huu wanavyokwenda kuwatumikia ili kuharakisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.Habari zinazofanana soma hapa.
Katibu Mkuu wa Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Hassan Kisabya na anayefuatia ni mgombea Urais  kwa tiketi ya NRA, Leopold Mahona wakizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali  vya habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, Leopard Lucas Mahona ameyasema hayo jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa ilani hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.

Mahona amesema kuwa, ilani hiyo ambayo inatekeleza itaenda kusimamiwa kikamilifu iwapo tu wananchi watakipa ridhaa chama hicho.

Mgombea urais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa,kipaumbele kikubwa ni kimoja tu ambacho ni takwimu kuhusu watu, vitu na mazingira.

Mbali na kipaumbele hicho amesema, vipo vipaumbele vingine vidogo 17 ambavyo ni pamoja na utawala bora, kilimo na mifugo, afya na ustawi wa jamii.

Amesema, vipaumbele vingine ni viwanda na mazingira, biashara na uchumi, utalii, madini, mafuta na gesi asilia, elimu, maji, umeme na makazi, uvuvi, usafirishaji, michezo na miundombinu.

Mahona amesema,katika Dunia ya sasa tunahitaji Serikali ya 'hardware na software' katika kuwatumikia Watanzania.  Amesema, Serikali ambayo inaweza kuwekeza kwenye miundombinu pamoja na zaidi katika rasilimali watu.

"Mfano ukijenga kituo cha afya ni lazima uhakikishe kwamba kuna vifaa tiba pamoja na watoa huduma wenye sifa stahiki,"amesema Mahona.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa chama hicho, Hassan Almas amesema, Serikali itakayoundwa na NRA itakuwa ni Serikali jumuishi ambayo itawashirikisha watu wa vyama vyote.

Amesema kuwa, kama watanzania watafanya maamuzi sahihi kwa kumchagua Mahona watakuwa wamefanya maamuzi ya busara ambayo yatawezesha wao kuzifikia ndoto zao kupitia maendeleo jumuishi na shirikishi kuanzia ngazi za chini hadi Taifa.

Amesema, Tanzania na watanzania wanahitaji kuwa salama kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu ili nchi iendelee kuwa na amani.

"Watanzania, Taifa ndio mama na baba yetu, tunahitaji Taifa zaidi ya kitu chochote, hivyo kila chama kinapaswa kuandaa malengo ya kuisaidia Tanzania na ndio maana NRA tumekuwa tukisisitiza Taifa kwanza vyama baadaye,"amesema.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu huyo amewataka Watanzania kuisoma ilani hiyo ili mwisho wa siku wafanye maamuzi sahihi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news