TCRA yatoa rai kwa MCT kuhusu vyombo vya habari

BARAZA la Habari Nchini (MCT) limeshauriwa kutoa ushauri kwa vyombo vya habari nchini pale panapotokea utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa maadili ya uandishi na utangazaji wa habari, anaripoti MWANDISHI WETU kutoka DAR ES SALAAM.

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Mhandisi James Kilaba mara baada ya kukifungia kutoa huduma za utangazaji kituo cha radio cha Wasafi kwa muda wa siku saba kuanzia Septemba 12 hadi Septemba 18,mwaka huu kutokana na kituo hicho kutozingatia maadili ya utangazaji

"Nitoe rai kwa MCT kama chombo kinachojishughulisha na masuala ya habari kuvionya vyombo vya habari pale panapotokea utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa maadili wa uandishi na utangazaji wa habari, "alisema Mhandisi Kilaba.

Mhandisi Kilaba, alivitaka vyombo vyote vya utangazaji na watangazaji wake kuzingatia kanuni zote za utangazaji kwa lengo la kulinda maslahi mapana ya nchi kimaadili.

Alisema kuwa,TCRA itaendelea kuchukua hatua zaidi ya hiyo ya kuvinfungia vyombo hivyo vya utangazaji,iwapo vyombo hivyo vitaendelea kukiuka sheria za utangazaji na kwamba kanuni za utangazaji ziwasaidie kimaadili.

"Ikumbukwe kwamba uamuzi wa namna hii siyo kiwango cha makosa mtakayoendelea kuyafunga, iwapo Wasafi itashindwa, itakataa au kukaidi uamuzi huu hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti zitachukuliwa dhidi yao, "alisema.

Alitaja kanuni namba 14 ya Kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta (Maudhui ya Utangazaji wa Radio na Televisheni ya mwaka 2018 zinatamka mtoa huduma anaapswa kuzingatia utangazaji wa maudhui yanayohusu watu wazima katika muda ulioruhusiwa kisheria.

Pia alisisitiza kwamba,mtoa huduma ya maudhui anapaswa kufuata sheria, kanuni na na masharti ya leseni sambamba na maelekezo yanayotolewa na TCRA katika utangazaji wa maudhui yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news