Waziri Pompeo akataliwa Vatican

Vatican imemkatalia Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo kuonana na Papa Francis. Kiongozi huyo wa juu wa Kanisa Katoliki ameelezwa kuwa, huwa hapokei wanasiasa wakati wa kipindi cha uchaguzi.

Hatua hiyo inaongeza hali ya mzozo wa kidiplomasia baada ya kauli ya Pompeo kuhusu China na Kanisa Katoliki.Vatican ilimtuhumu Pompeo kuwa anajaribu kutumia suala hilo kuvutia wapiga kura wa uchaguzi wa urais wa Novemba 3,mwaka huu nchini Marekani.
Katika makala ya mwanzoni mwa mwezi Septemba,mwaka huu Waziri Pompeo alisema Kanisa Katoliki linapoteza mamlaka yake ya kinidhamu kwa kufanya makubaliano mapya na China kuhusu uteuzi wa maaskofu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news