Afisa Mwandamizi ACT-Wazalendo kizimbani kwa kusambaza picha zenye maudhui ya ngono mtandaoni

Dotto Rangimoto (34) ambaye ni Afisa Habari Msaidizi wa Chama cha ACT-Wazalendo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kusambaza picha zenye maudhui ya ngono mtandaoni, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rangimoto amefikishwa leo Oktoba 6,2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega wa Mahakama hiyo kwa tuhuma za shtaka moja.

Wakili wa Serikali, Ashura Mzava akisoma hati ya mashtaka amedai kuwa, Dotto Rangimoto alitenda kosa hilo kati ya Januari Mosi hadi Februari 26,2020 eneo la Tabata wilayani Ilala,Dar es Salaam.

Mzava amedai kuwa, mshtakiwa huyo anatuhumiwa kusambaza picha za ngono akitumia simu ya mkononi aina ya Tecno T301 kwenye akaunti ya Twitter yenye jina la James Michael @James Michael kinyune cha sheria nchini.

Aidha, baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo, ambapo upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Katika hatua nyingine, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega amedai kuwa, ili mshtakiwa awe nje kwa dhamana anatakiwa awe na mdhamini mmoja wa kuaminika atakayesaini bondi ya shilingi milioni tano ambapo Rangimoto aliweza kutimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana. Hata hivyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 2, mwaka huu itakapotajwa tena na kuangalia kama upelelezi umekamilika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news