Huu ndiyo uzi mpya wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu watua nchini


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi leo Oktoba 6, 2020 ameshiriki uzinduzi wa jezi mpya za Timu ya Taifa (Taifa Stars) uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza kwenye uzinduzi wa jezi mpya za Timu ya Taifa ( Taifa Stasz) uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Oktoba 6,2020.

Katika uzinduzi huo pia Kampuni ya Bia ya Serengeti imeongeza mkataba wake wa udhamini kwa Timu ya Taifa wenye thamani ya shilingi bilioni tatu.

NYOTA WAINGIA NCHINI

Tayari nyota wa Kimataifa Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wameingia nchini leo kwa ajili ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya inayojiandaa na mchezo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Burundi, Oktoba 11.

Samatta kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya Fenerbahce ambayo inashiriki Ligi Kuu ya nchini Uturuki na tayari amecheza mechi mbili akiwa ametupia mabao mawili.

Samatta amesema kuwa, anaamini Tanzania itapata matokeo chanya kwenye mchezo huo wa kirafiki. Amesema, utakuwa mchezo mgumu na anaamini kwamba, mwalimu atakuwa na mpango mkubwa katika kuwapa matokeo mazuri.

Mbwana Samatta akiwasili nchini kwa ajili ya maandalizi.

Naye Thomas Ulimwengu anayekipiga TP Mazembe ya Congo, amewasili mchana wa leo tayari kuungana na wenzake wa Kikosi cha Taifa Stars akiwemo Mbwana Samatta aliyefika mapema leo.

Thomas Ulimwengu akiwasili kwa ajili ya maandalizi.

Taifa Stars inayonolewa na Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije iliingia kambini Oktoba 5, 2020 ikiwa tayari kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa Jumapili ya Oktoba 11, 2020, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news