KMC FC YATOA SABABU KUHAMISHA MECHI YA YANGA UWANJA WA MKAPA NA KUPELEKA CCM KIRUMBA MWANZA

Uongozi wa timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC umehamisha mchezo wake dhidi ya Yanga SC ambao ulikuwa ufanyike Oktoba 25 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na hivyo sasa utapigwa katika Dimba la CCM Kirumba jiji Mwanza,anaripoti Christina Mwangala (KMC FC).
Hatua hiyo inatokana na kutumia nafasi ambayo ilipitishwa na Bodi ya Ligi katika kikao chake cha ufunguzi wa ligi kuu Tanzania Bara ambapo ilieleza kuwa timu yeyote inaruhusiwa kucheza michezo yake miwili ya nyumbani nje ya kituo mama na hivyo kama KMC FC kutumia nafasi hiyo kupeleka mchezo huo jijini Mwanza.

Mbali na hivyo KMC FC pia inatambua thamani ya mashabiki waliopo katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kwamba wana lengo la kutoa burudani kwa kila eneo ambalo wanamashabiki hivyo katika awamu hii wameona ni muhimu kupeleka burudani hiyo kwa mashabiki waliopo mkoani humo.

“Tunafahamu kuwa tuna mashabiki wengi kwenye kila mkoa, hivyo ni nafasi kwa watu wa Mwanza kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kushuhudia soka safi linalochezwa na timu ya KMC FC na hivyo itakuwa ni salamu tosha kwa timu nyingine kongwe kuona ubora wa kikosi hicho,"amesema.

Hata hivyo KMC FC inawasishi mashabiki na wapenzi wa timu hiyo waliopo katika mikoa ya karibu na jiji la Mwanza na maeneo mengine kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 mwaka huu katika kuhakikisha kwamba wanakuja kushuhudia timu yao itakavyofanya vizuri na hivyo kuibuka na matokeo yenye viwango dhidi ya mchezo huo na Yanga.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news