Katibu Mkuu CCM Taifa asema wamejipanga vema, ateta na wazee Zanzibar

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Bashiru Ally amesema kuwa, chama hicho kimejipanga vyema katika uchaguzi mkuu na hakuna atakayetumia fedha zake kununua wapiga kura, kwani ni mwiko kwa mwana CCM kutumia fedha kurubuni wapiga kura.

Dkt.Bashiru ameyasema hayo leo Oktoba 5, 2020 katika mkutano wake na Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinzuzi (CCM) Zanzibar.

Mkutano uliofanyika katika Ofisi Kuu za chama hicho Kisiwandui, Unguja jijini Zanzibar ambapo amesema, kampeni za CCM zinaendeshwa kwa misingi minne ambayo ni kujitegemea, nidhamu, ajenda ya uchaguzi na kuwa na wagombea wanaoweza kuanza na kufika mwisho wa uchaguzi.
“Chama kina nguvu ya kuunganisha Watanzania ndiyo dhambi yetu, tuna viongozi wenye msimamo wa kulinda rasilimiali za nchi hii ndiyo dhambi yetu, tumeapa kuulinda Muungano wa Serikali mbili kwa gharama yoyote ndiyo dhambi yetu.

“Ukiona mtu anatafuta kura na anatembeza bakuli za pesa, unajiuliza anaomba kura au anaomba pesa? Ujue huyo hajajiandaa, kwa sababu Uchaguzi ulijulikana tangu 2015,”amesema Dkt.Bashiru.

 
Pia amesema, chama kinathamini na kuzienzi juhudi za wazee, kwani walitumia nguvu zao katika chama wakati wa ujana wao hivyo chama kitaendelea kuwatunza wazee hao.

“Yote ninayoyasema kuhusu maslahi ya wazee, maisha ya wazee, makazi ya wazee, huduma kwa wazee yameainishwa katika Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news