Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania yakanusha madai ya Tundu Lissu
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekanusha madai kuwa ilikataa kutoa kibali cha kuruka kwa helikopta ya Tundu Lissu kutoka KIA kwenda Dar es Salaam. Mamlaka hiyo imesema ombi la awali lililowasilishwa lilikuwa na mapungufu na mara yaliporekebishwa, walitoa kibali ndani ya dakika 12.