Manchester United yacharazwa bakora 6-1

Ukweli upo hivi, Manchester United wamejuta kucheza ndani ya Old Trafford dhidi ya Tottenham leo Oktoba 4,2020, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ni baada ya kujikuta katika wakati mgumu kwa kufungwa goli 6-1 na Tottenham ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Soka England.

Manchester United imefungwa magoli manne katika kipindi cha kwanza....

Manchester United chini ya Ole Gunnar Solskjaer waliwachokoza Spurs kwa bao la Bruno Fernandes kwa penalti 2'.
 
Tottenham ikazinduka kwa mabao ya Tanguy Ndombele 4', Heung-min Son mabao mawili 7' 37', Harry Kane 30' na 79' kwa penalti na Serge Aurier  51' hiyo ikawa ndiyo historia ya nusu dazeni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news