Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), Dkt.Wilson Mahera Charles amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura vimeongezwa katika baadhi ya majimbo hapa nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Dkt.Charles amesema kuwa, uvumi huo unalenga kuchafua mchakato wa uchaguzi ikiwa zimebaki siku chache kabla ya Watanzania zaidi ya milioni 28.1 kumiminika vituoni kuwachagua madiwani, wabunge na Rais.
Hayo ameyasema leo Oktoba 25, 2020 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt.Charles amesema kuwa, hakuna vituo hewa vya kupigia kura nchini huku akisema huo ni upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa siasa kutangaza kuwa kuna vituo hewa.
Amesema,anashangaa kuona taarifa za uzushi zikisambaa kwenye mitandao na baadhi ya viongozi wa vyama kuanza kulalamika na kuzusha kuwa NEC imeongeza vituo hewa vya kupigia kura nchini jambo ambalo halina ukweli wowote.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa yua Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani jarida la maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020 katika ofisi za tume zilizopo Njedengwa jijini Dodoma leo Oktoba 25,2020 wakati akifafanua kuhusu madai ya uwepo wa vituo na wapiga kura hewa katika maeneo mbalimbali nchini ambayo yamekua yakitolewa na vyama vya siasa na wagombea wao. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpigakura, Dkt.Cosmas Mwaisobwa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa yua Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani jarida la maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020 katika ofisi za tume zilizopo Njedengwa jijini Dodoma leo Oktoba 25,2020 wakati akifafanua kuhusu madai ya uwepo wa vituo na wapiga kura hewa katika maeneo mbalimbali nchini ambayo yamekua yakitolewa na vyama vya siasa na wagombea wao. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpigakura, Dkt.Cosmas Mwaisobwa. "Hawa wanaojaribu kutoa taarifa za uongo na kutaka kuwatisha wananchi wana nia ovu kwa nchi,watu wasitishike na taarifa za mtandaoni,"amesema Dkt.Charles. Pia amewataka wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo kuhakikisha vifaa vya uchaguzi vinasambazwa katika vituo vyote kwa wakati ili kuepuka migogoro inayoweza kuhatarisha uvunjifu wa amani katika kipindi cha uchaguzi Oktoba 28,mwaka huu.
Amesema,mchakato wa uchaguzi umegharimu fedha nyingi ambapo kwa upande wa daftari la wapinga limegharimu shilingi bilioni 157 na uchaguzi utagharimu sh.bilioni 331 na kwamba hadi sasa zimetumika bilioni 276 na fedha zote zimetoka kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za tume Njedengwa jijini Dodoma leo Oktoba 25, 2020 kuhusiana na madai ya uwepo wa vituo na wapiga kura hewa katika maeneo mbalimbali nchini ambayo yamekua yakitolewa na vyama vya siasa na wagombea wao.Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpigakura, Dkt.Cosmas Mwaisobwa.
Dkt.Charls amefafanua kuwa, kituo cha kupigia kura kinakuwa na wapiga kura kuanzia 450 hadi 500, hivyo kama watu 2,000 wamejiandikisha kwenye kituo kimoja wanagawanywa katika vituo vinne hadi vitano.
"Vituo sasa vitakavyotumika kupigia kura Tanzania bara ni 80,155 sasa tunashangaa baadhi ya vyama vya siasa vinasikika kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vikitoa tuhuma za uwepo wa mamilioni ya wapiga kura na vituo hewa,"amesisitiza.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ofisi za tume Njedengwa jijini Dodoma leo Oktoba 25, 2020 kuhudiana na madai ya uwepo wa vituo na wapiga kura hewa katika maeneo mbalimbali nchini ambayo yamekua yakitolewa na vyama vya siasa na wagombea wao.
Dkt.Mahera amesema kuwa,vituo vya kujiandikishia vilikuwa 37,814, lakini vituo vya wapiga kura sasa ni 80,155 kwa upande wa Tanzania Bara na vitakavyotumika Zanzibar ni 1,412 huku akisema, idadi ya vituo wamevikabidhi kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi mwaka huu.