Tanzania yazidi kupewa alama za juu kwa kuendesha uchaguzi huru na haki, TRW watoa tathimini

Taasisi ya THE RIGHT WAY (TRW) ambayo ilikuwa inahusika na utoaji elimu ya mpiga kura na kutazama Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu na kuhakikisha kuwa wa haki na usawa imesema uchaguzi ulikuwa wa haki na usawa kwani wengi walifuata utaratibu uliowekwa bila kuvunja sheria, anaripoti Mwandishi Diramakini.

TRW ilifanya utazamaji wa Uchaguzi Mkuu katika mikoa 10 ya Tanzania Bara ambayo ni Dar es Salaam, Tanga, Simiyu, Mwanza, Katavi, Geita, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Mtwara na Mbeya.

Akizungumza leo Oktoba 31,2020 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu TRW, Wallace Mayunga amefafanua kuhusu hali ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 28,2020 ambapo ameeleza kwamba uchaguzi mkuu umefanyika na washiriki wote wameepuka hali ya rushwa na udanganyifu,kuna upatikanaji sawa wa rasilimali za taifa kwa wagombea wote wa vyama vyote vya siasa.

"Uchaguzi umefanyika katika mazingira ya amani na hakuna fujo wala vitisho, kuna fursa sawa za matumizi ya vyombo vya habari vya umma na binafsi kwa vyama vyote vya siasa pia kulikuwa na mazingira mazuri kwa wapiga kura kupata haki yao ya kupiga kura hasa tume imerahisisha kwa kuwepo kwa vituo vingi vya kupigia kura ili kila mmoja aweze kupata haki yake ya msingi,"amesema Mayunga.
Mkurugenzi Mkuu wa TRW, Wallace Mayunga akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam akielezea kuhusu utazamaji wa hali ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 28,2020 na kufafanua zaidi kuwa uchaguzi mkuu umefanyika na washiriki wote wameepuka hali ya rushwa na udanganyifu sambamba na upatikanaji sawa wa rasilimali za taifa kwa wagombea wote wa vyama vyote vya siasa.

Mayunga amesema, pamoja na changamoto za rasilimali fedha, lakini wameweza kuifikia mikoa 10 kwa kuweka watazamaji ambapo walifanya kazi hiyo na sasa wanaendelea kuwasilisha taarifa zao kwao ambazo zitasaidia katika kuandika taarifa yao kuu.

Pamoja na hayo Mayunga ametoa pongezi kwa Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama kwani vimepiga hatua kuhakikisha usalama wa nchi na wapiga kura uliimarishwa kipindi chote cha Uchaguzi.
Afisa Programu, Uchaguzi na Elimu ya Mpiga Kura kutoka Taasisi ya THE RIGHT WAY (TRW) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati akimkaribisha Mkurugenzi wa tasisi hiyo kuzungumza na wanahabari kuhusu hali ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 28,2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news