Zitto Kabwe aanza safari kwa matibabu zaidi

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiwasili uwanja wa ndege Kigoma kwa ajili ya safari ya kwenda Dar es Salaam kwa matibabu zaidi, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli amempigia simu ndugu Zitto Kabwe na kumpa pole huku akimuombea kwa Mwenyenzi Mungu apone haraka.

Endelea kufuatilia hapa tutakujuza hatua kwa hatua...

Kwa mujibu wa Chama cha ACT Wazalendo, baadaye majeruhi wote watapokelewa na gari la wagonjwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi. 

Mbali na Zitto, majeruhi wengine ni pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Said Rashid Bakema., Katibu wa Jimbo la Kigoma Kusini, Soily Simon Matetepamoja na Boaz Chuma, (mwanachama).

"Ninaendelea vizuri. Ilikuwa ajali mbaya sana. Namshukuru Allah kwa kutuponya. Shukran Wahudumu wa Kituo cha Afya Kalya, licha ya changamoto, Huduma ya kwanza imetusaidia. Shukran Madaktari na Wahudumu Hospitali ya Maweni Kigoma. Mimi na wenzangu, mpaka sasa, ni wazima,"ameeleza Zitto Kabwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news