Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Mei 12,2024

MOROGORO-Watu watano wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kutenda makosa ya ukatili wa kijinsia ya kubaka na ulawiti watoto wadogo , wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari katika Manispaa ya Morogoro na Wilaya ya Malinyi.Kamanda wa Polisi mkoa huo, Alex Mkama alitaja tukio la kwanza liliotokea Aprili14, mwaka huu katika kijiji cha Njiwa Wilaya ya Malinyi ambapo Juma Said (23) mkulima na makazi wa Njiwa alikamatwa kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa shule ya Msingi mwenye umri wa miaka 13.
Mkama, alitaja tukio lingine lilitokea Mei 3, mwaka huu ambapo polisi ilimtika mbaroni Tonny Myolele (17) mwanafunzi na mkazi wa Kata ya Ngoherenga Wilaya ya Malinyi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi mwenzake wa shule ya sekondari Ngoheranga mwenye miaka (15).Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news