CHADEMA waandamana, wataka Mdee na wenzake 18 wafukuzwe

Wakati leo Novemba 27,2020 macho na masikio ya Watanzania yakiwa yametegwa makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kufahamu juu ya maamuzi ya Kamati Kuu dhidi ya wabunge wa viti maalum walioapishwa na kudaiwa ni batili, muda mfupi baadhi ya wanachama wa chama hicho wakiwemo wajumbe wa Baraza la Wanawake la chama hicho (BAWACHA) wametinga makao makuu na mabango, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Wanachama hao wakiwa nje ya ofisi za makao makuu Mtaa wa Ufipa uliopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam wamebeba mabango wakishinikiza chama hicho kuwafukuza uanachama makada hao 19 wa chama hicho.

Makada hao ambao ni wabunge wa Viti Maalum waliapishwa hivi karibuni katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma wakiongozwa na Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa, Halima Mdee.

Wengine ni Asia Mohamed, Felista Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Simon, Anatropia Theonest,Salome Makamba, Conchester Lwamraza, Grace Tendega, Ester Matiko,Secilia Pareso,Ester Bulaya, Agnes Kaiza, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo.

Hata hivyo, makada hao wanahojiwa na Kamati Kuu ya chama hicho kuhusu uamuzi wao wa kwenda kula kiapo wakati mchakato wa kupeleka majina yao ukiwa haujafanyika na hayana baraka zozote.

Post a Comment

0 Comments