HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI YA KWANZA KWA UBORA AFRIKA 2020

Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda tuzo ya kuwa Hifadhi Bora katika Bara la Afrika kwa mwaka 2020, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Tuzo hiyo imetangazwa Novemba 9,2020 na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kwa njia ya mtandao.

Hii ni mara ya pili kwa Hifadhi ya Taifa Serengeti kushinda katika Kundi la Hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi Bara la Afrika baada kushinda pia mwaka 2019.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA), Pascal Shelutete amethibitisha.

Shelutete amesema, Serengeti imeibuka na ushindi katika shindano hilo lililoshindanisha hifadhi nyingine za Central Kalahari (Botswana); Etosha (Namibia); Kidepo Valley (Uganda): Kruger (Afiika ya Kusinl) na Maasai Mara National Reserve (Kenya).
Amesema, Serengeti inajivunia umaarufu wa msafara wa nyumbu wahamao zaaidi ya milioni moja na nusu na aina mbalimbali za wanyamapori wanaopatikana kwa wingi.

"Serengeti ina mandhari nzuri ya kuvutia pamoja na shughuli mbalimball za utalli zinazovutia watalli wengi. Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi, Wadau wa Utali pamoja na wale wote waliotumia muda wao kupiga kura na kuifanya Serengeti kuwa mshindi wa Hifadhi Bora zaidi kwa Bara la Afrika kwa mwaka 2020," amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news