Rais Magufuli kulihutubia Bunge la 12, Taifa


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli atalihutubia Bunge la 12 Ijumaa ya Novemba 13, 2020 saa 3:00 asubuhi jijini Dodoma, kuashiria kuanza rasmi kwa Bunge.

Mheshimiwa Ndugai ameyasema hayo leo Novemba 11, 2020 bungeni jijini Dodoma.

"Naomba wabunge wote muwepo, Rais atalihutubia Bunge, lakini kupitia sisi atakuwa akihutubia Taifa,"amesema Spika Ndugai. (Imeandaliwa na Mwandishi Diramakini).

Post a Comment

0 Comments