Huyu ndiye Hassan Mwakinyo aliyemchapa makonde Jose Carlos Paz

Promota Kelvin Twissa akimuinua bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo baada ya kumshinda Muargentina, Jose Carlos Paz kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya nne na kuetetea taji lake la WBF Intercontinental uzito wa Super Welter usiku wa jana Novemba 13, 2020 katika ukumbi wa Next Door Arena, Masaki jijini Dar es Salaam,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Matokeo hayo ni baada ya hatua hizi, “Nimehama nyumbani na kujichimbia huku Magoroto kwa lengo la kufanya vyema katika pambano hilo, kujifua zaidi ya raundi 12 ili kupata stamina ya kwenda sambamba na mpinzani wangu;

Hassan Mwakinyo aliyasema hayo akiwa katika mazoezi makali kwa ajili ya kujiandaa kumkabili bondia Jose Carlos Paz kutoka Argentina

Mwakinyo kabla ya mpambano wa jana aliweka kambi eneo la Magoroto mjini Muheza mkoani Tanga kuelekea pambano la kutetea ubingwa wa mabara wa WBF na kuwania ubingwa mpya wa mabara wa IBA wa uzito wa super-welter.

Bondia huyo alikuwa anajifua chini ya kocha, Hamis Mwakinyo pamoja na wasaidizi mbalimbali huku wakitumia video mbalimbali kumsoma Paz ambaye ana rekodi nzuri.
 
Naye bondia Jose Carlos Paz wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere alitamba kutwaa ubingwa wa uzito wa Weight Super Welter (WBF) unaoshikiliwa na Hassan Mwakinyo

Paz ambaye aliwasili na baba yake Alberto Ramon Paz ambaye pia ni kocha wake kama ilivyo kwa bondia Floyd Mayweather alisema kuwa, amesafiri umbali mrefu kwa ajili ya kutwaa ubingwa katika pambano hilo linalojulikana kwa jina la Jackson Group Fight Night.
 
 Paz alisema kuwa, amechukua tahadhari kubwa kwa ajili ya Mwakinyo na kwamba siyo bondia mbaya. “Nimefika mapema zaidi ili kuzoea hali ya hewa, hii ni moja ya mikakati ya ushindi, nilisafiri kwa basi na baadaye kupanda ndege, siku mbili nipo njiani, sitakuwa tayari kushindwa katika pambano hili,”amesema Paz.

Kocha wake, Alberto Ramon naye alisema kuwa, wamemsoma Mwakinyo katika mapambano yake na kujua mbinu zake ambazo amezifanyia kazi. “Tumefanya mazoezi magumu kuelekea pambano hili, tumefanya mazoezi ya ufundi na mbinu, hayo yote ni kwa ajili ya kusaka ushindi ambao tunaamini asilimia 100, tutashinda,”amesema Ramon. Mwakinyo afanya zoezi kali kumchapa Paz.

Post a Comment

0 Comments