Makamu wa Rais mgeni rasmi NBC Marathon

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya NBC Marathon,anaripoti Doreen Aloyce, Dodoma

Mshindano hayo yanatarajiwa kufanyika kesho katika viwanja vya Jamhuri yakiwa na lengo kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.Pia licha ya kuwa mgeni rasmi pia atakuwa kama mshiriki wa mbio hizo ambapo anatarajiwa kukimbia kilomita tano.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Yusuph Singo amesema mashindano hayo yatahusisha washiriki 3,000.

Amesema, mashindano hayo yameganyika kulingana kilomita walizochagua washiriki.

“Mbio zimegawanyika katika makundi matano, kuanzia km4, km5, km10 km 21 na km 42 ambapo itahusisha washiriki ambao nimewataja ambao miongoni mwao 35 wanatoka nchini Kenya, Uganda,na Malawi,"amesema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa  Benki ya NBC, William Kallaghe amesema benki hiyo imetenga sh.milioni 45.4 kwa ajili ya zawadi kwa washindi wa mbio hizo.

Amesema, lengo la kutenga kiasi cha fedha hizo no kufanya mashindano hayo kuwa na hadhi ya kimataifa.

“Tumeandaa zawadi kwa washindi pamoja na burudani za kutosha zitakazotolewa na wasanii ambapo hadi sasa tayari wamethibitisha ushiriki wao. Wasanii hao ni pamoja na Raivan,Kala Jeremaya na Bushoke ambao watakuwa wanatoa burudani wakati wanasubiriwa washiriki wanaokimbia mbio ndefu,"amesema.

Post a Comment

0 Comments