Makombora yatumika kulipiza visasi Ethiopia

Serikali ya Jimbo la Tigray Kaskazini mwa Ethiopia imetangaza kwamba mashambulio ya makombora ndani ya jimbo la Amhara ni ulipizaji kisasi wa mashambulio ya ndege yaliyofanywa na jeshi la serikali kuu jimboni humo hivi karibuni.

Serikali ya Addis Ababa ilitoa taarifa Jumamosi ikieleza kwamba , roketi mbili ziliharibu sehemu ya uwanja wa ndege wa Gondar jimboni Amhara, Ijuma usiku na moja ikikosa shabaha yake kwenye uwanja wa ndege wa Bahir Dar.

Jeshi la Ethiopia limekua likipambana na wapiganaji wa jimbo hilo kwa zaidi ya wiki moja na inaripotiwa mamia ya watu wamefariki tangu Waziri mkuu Abiy Ahmed kupeleka majeshi huko Novemba 4, 2020.

Mapigano yamewasababisha maelfu ya watu kukimbia katika nchi jirani ya Sudan na Eritrea wakidai kuwepo na mateso na hali ya wasiwasi.

Mkuu wa kimkoa wa Idara ya Wakimbizi ya Sudan, Alsir Khaled amesema, Ijuma kwamba kuna waethopia elfu 21 walovuka mpaka, wengi vijana, walikua na njaa na wamechoka baada kutembea kwa siku kadhaa.

Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameeleza Ijumaa jinsi alivyoshtushwa na namna hali ilivyozorota haraka huko jimboni Tigray.

Msemaji wake, Rupert Colville anasema, Bachelet amekerwa zaidi na ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty Internationl kuhusu tuhuma za mauaji ya halaiki huko Mai-Kadra Kusini Magharibi mwa Tigray.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news