Katibu Mkuu mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Patrick Mbundi amesema kuwa katika nafasi yake hiyo ataanza na vipaumbele muhimu ikiwemo kuimarisha soko la pamoja, kukuza biashara ya pamoja ndani nje ya nchi.
Ameyasema hayo jijini Arusha katika hafla ya makabidhiano ya madaraka baina yake na Katibu mkuu aliyemaliza muda wake,Veronica Nduva hafla iliyofanyika katika makao makuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Balozi Mbundi amesema kuwa, atahakikisha kuna kuwepo usimamizi thabiti wa rasilimali, uwajibikaji na uwazi katika utekelezaji wa majukumu ya jumuiya kwa ujumla.
“ninachoomba kwa wanajumuiya wenzangu ni ushirikiano wa karibu ili niweze kufanikisha malengo yote niliyotapanga na kukabiliana na changamoto mbalimbali,”amesema Mbundi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













