Mwakinyo amkaribia Manny Pacquiao kwa ubora Duniani

Mwanamasumbwi wa Kimataifa, Mtanzania Hassan Mwakinyo ametajwa kuwa bondia wa nyota tatu duniani, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mwakinyo anahitaji kutafuta nyota nyingine mbili ili kuingia anga za mabondia wanaotamba duniani akiwemo Manny Pacquiao mwenye nyota tano kwa sasa.

Kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa na mtandao wa ngumi za kulipwa wa Dunia, Boxrec,Mwakinyo amepanda kutoka nafasi ya 78 hadi ya 41 duniani kati ya mabondia 2,050 wa uzani wa Super Welter.

Aidha, bondia huyo licha ya kushinda mapambano kadhaa mwaka huu likiwemo la Tshibangu Kayembe, alibaki nafasi ya 78 mpaka sasa vilipotajwa viwango vipya na kupanda hadi nafasi ya 41.

Wachambuzi wa masuala ya masumbi wamemdokeza Mwandishi Diramakini kuwa, hatua hii ya Mwakinyo kuingia katika mabondia 50 bora duniani ni kubwa na hivyo anapaswa kuongeza bidii ikiwemo kumtegemea Mwenyenzi Mungu na hakika atafanya maajabu siku za usoni.

Post a Comment

0 Comments