Yanga SC yawachapa JKT Tanzania 1-0

Klabu ya Yanga imeendelea kujiimarisha zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya leo kuwachapa maafande wa JKT Tanzania 1-0, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mtanange huo umepigwa leo jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam ambapo kiungo Deus Kaseke dakika ya 33 alimalizia pasi ya Yacouba Sogne, bao ambalo lilidumu hadi dakika tisini.

Chini ya kocha wao, Cedric Kaze, Yanga SC inafikisha alama 31 baada ya kucheza mechi 13 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa alama sita mbele ya Azam FC huku watani wao Simba SC wakiwa nafasi ya tatu.

Mchezo huo ulichezeshwa na Refa Abel William wa Arusha, aliyesaidiwa na Sunday Komba wa Kilimanjaro na Hamdan Said wa Mtwara ambapo kikosi cha Yanga kiliundwa na Metacha Mnata, Paul Godfrey ‘Boxer’/Abdallah Shaibu ‘Ninja’ dk70, Yassin Mustapha, Said Juma ‘Makapu’, Bakari Mwamnyeto, Tonombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Feisal Salum/Zawadi Mauya dk55, Ditram Nchimbi, Deus Kaseke na Yacouba Sogne/Farid Mussa dakika ya 55.

Wakati upande wa JKT Tanzania kikosi kiliundwa na Joseph Ilunda, Michael Aidan, Hassan Twalib, Edson Katanga, Nurdin Mohammed, Jabir Aziz, Shaaban Mgandila, Hafidh Mussa, Daniel Lyanga,Kelvin Nashon/Ally Bilal dakika ya 76 na Adam Adam/Mohamed Rashid dakika ya 81.

Post a Comment

0 Comments