Magazeti leo Juni 20,2026

MFUKO wa SELF Microfinance Fund umetumia Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma kuhamasisha wananchi, wajasiriamali, wakulima na wafugaji kunufaika na huduma zake za mikopo na elimu ya fedha, hatua inayolenga kuongeza ushiriki wao katika shughuli za uzalishaji na maendeleo ya uchumi.
Hayo yamesemwa Juni 18, 2026 na Meneja wa Mfuko wa SELF Kanda ya Kati, Aristid Tesha, katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, ambapo taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu na huduma mbalimbali kwa wananchi wanaotembelea banda lake.

Tesha amesema kanda hiyo inahudumia mikoa ya Dodoma na Singida na kwamba ushiriki wa SELF katika maonesho hayo unalenga kuwafikisha wananchi karibu na huduma zake pamoja na kuwawezesha kufahamu fursa zilizopo kwa ajili ya kukuza shughuli zao za kiuchumi.

Amesema tangu kuanza kwa maonesho hayo Juni 16, wananchi wengi wamejitokeza kutembelea banda la SELF kwa lengo la kupata elimu ya ujasiriamali, usimamizi wa fedha na taarifa kuhusu huduma mbalimbali za mikopo zinazotolewa na mfuko huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here