Nangwanda Sijaona Stadium yashindwa kubeba mashabiki wa Harmonize leo

Ni mafuriko, ndivyo unavyoweza kusema baada ya Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kufurika maelfu ya watu katika tamasha la Harmonize, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Sehemu ya mashabiki wa Harmonize usiku huu hapa Nangwanda Sijaona Stadium mjini Mtwara. (Diramakini).

Diramakini imeshuhudia katika uwanja huo, licha ya angalizo la Afisa Mtendaji Mkuu wa Konde Gang, Rajabu Abdul Kahali (Harmonize) kuwataka kusitisha kuingia uwanjani hapo kwa hofu ya watu kukosa hewa, mamia wameendelea kuingia

"Kutokana na tatizo la uwanja kuwa mdogo nasikitika kuwajuza ndugu zangu wa Mtwara kuwa, hairuhusiwi kuingia mtu kuanzia now, so kama upo nyumbani basi baki tu huko huko.

"Usisumbuke wa nje ni wa nje na wa ndani ni wa ndani, tutaonana wakati mwingine... Inshallah,"Harmonize amewaeleza maelfu ya wafuasi wake.

Hata hivyo, licha ya angalizo hilo mamia ya watu wanazidi kufurika katika uwanja huu wa Nangwanda Sijaona Stadium hapa mjini Mtwara.

Post a Comment

0 Comments