Rais Magufuli awateua Profesa Kabudi na Dkt.Mpango kuwa mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Mawaziri wawili katika Baraza jipya la Mawaziri, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya ndugu, Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU leo Novemba 13, 2020 katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Amesema,Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Pili, Rais Magufuli amemteua Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango. Mawaziri Wateule hao walikuwa wakishikilia nyadhifa hizo katika Baraza la Mawaziri lililopita na uteuzi huu unaanza leo tarehe 13 Novemba, 2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news