Samuel Eto’o anusurika kifo katika ajali

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon na Klabu ya FC Barcelona ya nchini Uhispania, Samuel Eto’o (39) amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari.
Straika huyo mstaafu ambaye alizaliwa Machi 10, 1981 nchini Cameroon anatajwa kuwa na ukwasi wa zaidi ya dola milioni 95 na mchezaji tajiri zaidi barani Afrika.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka mjini Bafoussam, Eto’o amepata ajali ya gari akitokea katika sherehe kwenye mji huo uliopo Magharibi kuelekea mji wa Douala nchini humo.

Post a Comment

0 Comments