Sherehe ya kuapishwa Rais Dkt.Magufuli Novemba 5, 2020

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiapishwa na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Tano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za Uapisho wake kuwa Rais wa Tanzania kwa Muhula wa Pili katika Awamu Tano zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwa ameshika Mkuki na Ngao mara baada ya kukabidhiwa na Wazee kama ishara ya Kukabidhiwa Madaraka na Ulinzi muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli akizungumza na Wananchi pamoja na Wageni Mbalimbali mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania kwa Muhula wa Pili katika Awamu ya tano katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa akitoa salamu za Wananchi wa Zimbabwe katika sherehe za Uapisho wa Rais wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza katika sherehe za Uapisho wa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za Uapisho wa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akipongezwa na Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa mara baada ya sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. (PICHA NA IKULU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiteta jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi muda mfupi mara baada ya sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada yakuapishwa katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news