Standard Chartered kwa kushirikiana na Sanlam yazindua bima bora

Benki ya Standard Chartered kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam wamezindua huduma ya bima za bidhaa kwa wateja ili kuongeza thamani kwa wateja wao, anaripoti Mwandishi Diramakini. 

Uzinduzi huo wa bidhaa za bima uliokwenda kwa kauli mbiu ya “Tunavilinda vyenye Tija,” umehusisha bidhaa mbalimbali ikiwemo nyumba na magari kwa ulinzi na usalama wa mali za wateja wao. 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani amesema kuwa, suala la bima limekuwa na manufaa kwa sasa kutokana na ulinzi na usalama kupitia bima za bidhaa mbalimbali ikiwemo magari, nyumba na afya.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Tanzania, Khamis Suleiman mara baada ya kuzindua huduma za bima za benki hiyo kwa ushirikiano na Kampuni ya Bima ya Sanlam ya jijini Dar es Salaam kwenye Hoteli ya Hyatt Regency.Kushoto ni Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ajmair Riaz. 

Amesema, Tanzania ni sehemu salama na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imekuwa ikishirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika kujenga uchumi wa Taifa. 

“Bima ina umuhimu mkubwa hasa katika ulinzi na usalama, watanzania lazima waelewe umuhimu wa kukata bima katika mabenki kwa manufaa yao binafsi na mali zao,”amesema. 

Amesema kuwa, huo ni ushirikiano wa kibiashara kwa maendeleo ya jamii na taifa la Tanzania na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendeleza bima zikiwemo za sekta ya madini na afya.  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sanlam Tanzania, Khamis Suleiman akielezea namna ushirikiano wa kampuni hiyo na benki ya Starndard Chatered zitakavyotolewa katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani na kushoto ni Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ajmair Riaz. 
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani akifafanua jambo mara baada ya uzinduzi wa huduma hizo za bima kushoto ni Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ajmair Riaz. 
Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akizungumza jambo mara baada ya uzinduzi wa huduma za bima zitakazokuwa zikitolewa na benki hiyo. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sanlam Tanzania, Khamis Suleiman  amesema, benki kuanza kuuza bima ni muhimu kwa kuwa wanafahamu ni nini mteja anacho na anachoweza kununua. 

Amesema kuwa, kampuni hiyo iliyotimiza miaka 102 tangu kuanzishwa kwake ina malengo ya kufikia asilimia 50 ya watanzania wanaomiliki bima hadi kufikia mwaka 2030, na bima hizo zikiwa ni pamoja na bima za nyumba na magari.  

Pia amesema, Sanlam imekuwa nchini kwa miaka 20, wakiwa katika nchi 44 zikiwemo nchi zote za Afrika Mashariki na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa ustawi wa jamii na taifa la Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news