TAKUKURU yaja kivingine, ukijilengesha umekwisha

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imeazimia kutatua kero za wananchi huku ikirejesha zaidi ya shilingi milioni 118 kwa mfadhili wa huduma za afya nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Brigedia Jenerali John Julius Mbungo. (MAKTABA).

"Kwa mara nyingine tena tumewaita hapa ili kupitia kwenu, tuendelee kuujulisha umma juu ya hatua mbalimbali za utekelezaji wa majukumu tunayoyatekeleza kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007;

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Brigedia Jenerali John Julius Mbungo ameyasema hayo leo Novemba 14, 2020.

"Tumekuwa tukifanya hivi mara kwa mara kwa kuwa ni jukumu la taasisi kuufahamisha umma wa Watanzania kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na TAKUKURU katika kuongoza mapambano dhidi ya rushwa hapa nchini," amesema Brigedia Jenerali John Julius Mbungo.

Amesema kuwa,TAKUKURU imejizatiti kutekeleza pamoja na mambo mengine, maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyokuwa akiyatoa katika maeneo mbalimbali wakati wa kampeni ya kugombea kiti cha urais, yanayohusu kero mbalimbali katika maeneo husika.
"Tunatoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwa utaratibu huu na tunatoa wito kwa wakurugenzi wengine kwamba waendelee kushirikiana na TAKUKURU katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha fedha za Serikali ambazo zinatokana na kodi za wananchi zinatumika kwa kadri ya malengo yaliyokusudiwa,"amesema.

(b) Vilevile kupitia Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Manyara tumefanya uchunguzi dhidi ya dhuluma iliyofanyika kwa wajasiriamali takribani 300 kutoka Wilaya ya Hanang' ambao walichangishwa shilingi 140,000 kila mmoja kwa ahadi ya kuanzisha biahara ya ufugaji wa kuku.

"Udanganyifu huu ulifanyika tangu mwaka 2016 ambapo kampuni moja ya biashara kwa kushirikiana na baadhi ya maafisa wachache wa Serikali wasio waadilifu ilijipatia shilingi milioni 42 kwa njia ya udanganyifu,"ameendelea kufafanua.
wametekeleza chini ya kiwango mradi wa ujenzi wa Bwawa la Lwanyo. TAKUKURU inaendelea na uchunguzi huu. Mpaka sasa tumebaini kwamba, ujenzi wa bwawa hilo umegharimu shilingi 2, 951,469,353.70 lakini kwa sasa bwawa hili halitumiki kama ilivyokusudiwa. Uchunguzi wa suala hili unaendelea na upo katika hatua za mwisho,"amesema.

"Wakandarasi hao walikuwa wakidai shilingi bilioni 1.3 na tayari TAKUKURU imewezesha Mkandarasi Mkuu kuhojiwa ili kueleza utaratibu wa kuwalipa wanaodai fedha zao,"amesema.
"Kero hizi na nyingine zote zitaendelea kushughulikiwa kwa kasi kubwa sana kama ambavyo leo hii mtashuhudia mwakilishi kutoka shirika moja la Kimataifa lisilo la kiserikali akirejeshewa fedha zaidi ya shilingi za Kitanzania milioni 118 ambazo zilikuwa zimechepushwa kwa njia ya udanganyifu,"amesema.

Brigedia Jenerali John Julius Mbungo amesema kuwa, wote ambao wanaojifahamu walichukua fedha za umma kwa njia ya za udanganyifu au dhuluma kwa wanyonge wanatakiwa wazirejeshe kabla rungu la TAKUKURU halijawafikia.

"Kama amabavyo, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameeleza wakati akizindua Bunge la 12 Novemba 13, 2020 (jana) amesema, ninamnukuu.

"Watumishi wazembe bado wapo, wala rushwa bado wapo. Wezi na wabadhirifu wa mali za umma bado wapo... utumbuaji majibu utaendelea,"Brigedia Jenerali John Julius Mbungo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAKUKURU amemnukuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news