Tetesi:Manchester City yaachana na Lionel Messi,Chris Wilder yupo tayari

Kwa mujibu wa Sky Sports, Chris Wilder, ambaye klabu yake ya Sheffield United ipo chini ya jedwali la Ligi ya Premia ikiwa na alama moja pekee anasisitiza kwamba haogopi kufutwa kazi katika klabu hiyo.

Manchester Evening News. inaripoti kuwa, jeraha la mguu la beki wa Barcelona na Uhispania Gerard Pique (33) huenda likabadilisha jinsi klabu hiyo itakavyomtafuta beki mwingine Januari, 2021.

Lengo likiwa ni kujaza pengo lake ambapo mabingwa hao wa Catalan wana hamu ya kumsajili beki wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia (19).

Sky Sports inadokeza tena kuwa, Klabu ya Manchester City imesitisha harakati zake za kutaka kumsajili mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi (33) ikiwa ni kwa mujibu wa mtaalamu wa soka wa Uhispania , Semra Hunter.

Wakati huo huo, Mirror inaripoti kuwa, mshambuiaji wa Ufaransa, Olivier Giroud (34) amekiri kukosa muda wa kushiriki katika mechi Chelsea kunamtia wasiwasi na kwamba huenda akafanya maamuzi kuhusu hatma yake ya siku zijazo kuznzia Januari, 2021. (Mirror)

Pia aliyekuwa kiungo wa kati wa Tottenham, Christian Eriksen (28) yuko huru kuondoka Inter Milan mwezi Januari, 2021 kwa mujibu wa Goal, afisa mkuu wa klabu hiyo ya Itali Beppe Marotta amethibitisha.

Katika hatua nyingine, Mirror inadokeza kuwa, Klabu ya Arsenal imepigwa jeki katika harakati zake za kumsajili kiungo wa kati wa Uturuki, Yusuf Yazici baada ya wakala wake kukiri kwamba mchezaji huyo huenda akaondoka katika klabu ya Lille. Mchezaji huyo amefananishwa na kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil (32).

Tuhitimishe na Sun ambayo inaripoti kuwa, kipa wa klabu ya Manchester United, Dean Henderson (23) atafuatilia uhamisho wake wa mkopo ili kuimarisha hadhi yake katika kushiriki kombe la mabingwa Ulaya huku klabu za Leeds na Brightong zikihusishwa na ununuzi wa mchezaji huyo mwezi Januari, 2021.

Post a Comment

0 Comments