Magazeti leo Aprili 8,2026

Mgogoro wa mpaka uliodumu kwa zaidi ya miaka 14 kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Wilaya ya Kilolo, unaohusisha vijiji vya Irole na Ilambilole, hatimaye umepatiwa ufumbuzi baada ya juhudi za pamoja za serikali.
Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya hizo, zikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamini Sita, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, zimefika katika eneo la tukio kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto hiyo iliyokuwa kikwazo kwa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.

Katika kikao kilichofanyika, wananchi kutoka pande zote mbili walipata nafasi ya kueleza malalamiko yao, huku wataalamu wa ardhi wakitoa ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu mipaka halisi ya maeneo hayo.

Baada ya majadiliano ya kina, uamuzi wa mwisho kuhusu mpaka ulitolewa, hatua inayotarajiwa kumaliza sintofahamu iliyodumu kwa muda mrefu na kurejesha utulivu pamoja na ushirikiano kati ya wananchi wa vijiji hivyo.

Akizungumza mara baada ya kufikiwa kwa muafaka huo, viongozi wa wilaya hizo wamesisitiza umuhimu wa wananchi kuheshimu mipaka iliyowekwa ili kuepusha migogoro ya aina hiyo kujirudia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here