Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh amewataka wakaguzi wa mazao ya uvuvi kufanya kazi zao kwa ubora ili kulisaidia Taifa kuongeza kiwango cha mazao ya uvuvi yanayosafirishwa nje ya nchi.
Prof Sheikh ametoa kauli hiyo Aprili 8, 2026 wakati akizindua mafunzo ya siku tano kwa maafisa wakaguzi wa mazao ya uvuvi 25 yaliyoandaliwa na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO).“Takwimu zinaonesha kwasasa tunasafirisha tani 60,000 pekee za samaki kwenda nje ya nchi hivyo uwepo wa mafunzo haya uwe chachu ya kuongeza ubora utakaosaidia Taifa kuongeza kiasi cha samaki kinachopelekwa nje ya nchi,” amesema Prof. Sheikh.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
















