Watanzania wapongezwa kwa kuishinda Corona

Watanzania wamepongezwa kwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababisha virusi vya Corona (COVID -19) ambapo wameweza kuushinda na kuufanya utoweke nchini,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kauli hiyo imetolewa na Mwinjilisti na Mkurugenzi wa Maandalizi ya Mkutano mkubwa wa injili, Randy Roberts wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tabora.

Amesema, Watanzania wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli wamefanikiwa kuondoa tatizo hilo na kuwawezesha kuendelea na shughuli mbalimbali.

“Watanzania hawakukubali kuupigia magoti ugonjwa wa COVID 19 badala yake walimuinua Mungu juu na hatimaye wamefanikiwa kuushinda, hongreni sana,”amesema.

Amesema, hali hiyo imewawezesha kuendelea na shughuli zinazowaunganisha watu pamoja ikiwemo mikutano ya injili na shughuli nyingine za ibada.

Roberts amesema, kutokana na uwepo wa mazingira salama nchini Tanzania wanatarajia kuendesha Mkutano Mkubwa wa Injili mkoani Tabora kuanzia wiki ijayo kwa ajili ya kuendelea kuwaombea watu wenye matatizo mbalimbali.

Mkurugenzi huyo amesema, katika baadhi ya nchi za jirani na Tanzania wameshindwa kuendesha mikutano ya injili kutokana na kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID -19)

Amesema, ndani ya wiki mbili zijazo wanatarajia kuwa na mikutano ya injili katika maeneo ya Singida, Arusha, Shinyanga, Tabora na Kahama ambapo Mwinjilisti Jared Horthon ataongoza katika kuwaombea wakazi wa maeneo hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news