ZFF:Mlandege FC dhidi ya timu CS SFAXIEN leo mashabiki hawataruhusiwa

 TAARIFA

Kulingana na Miongozo iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF juu ya kuendelea kujikinga na COVID 19  michezoni hasa katika michezo ya kimataifa mchezo wa leo wa Klub Bingwa Africa unaotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Amaan majira ya Saa 10:00 Alasiri kati ya Mlandege FC dhidi ya timu CS SFAXIEN  ya nchini Tunisia mchezo huo hawataruhusiwa kuingia mashabiki uwanjani.

CAF imeruhusu watu 200 tu ambao watakaa katika eneo la VIP Kwa kufuata miongozo yote ya Kiafya ya kujikinga na  COVID -19.

Post a Comment

0 Comments