Beki Motjeka Madisha afariki

Beki wa Mamelodi Sundowns, Motjeka Madisha (25) amefariki leo Desemba 13, 2020 kutokana na ajali iliyotokea mjini Johannesburg, Afrika Kusini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Madisha ameichezea Mamelodi zaidi ya mechi 130 na kushinda makombe matatu ya ligi kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika na Super Cup. 

Beki huyo ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa tegemeo kwenye mafanikio ya Mamelodi chini ya kocha Pitso Mosimane, ambapo mbali na ligi pamoja na klabu bingwa pia walishinda mataji mbalimbali kama Telkom Knockout, the Nedbank Cup. Aidha,nyota huyo ameichezea timu ya taifa ya Afrika Kusini. 

Beki Motjeka nyota wa tisa kufariki katika ajali ya gari tangu 2003 wengine waliofariki ndani ya kipindi hicho hadi sasa ni;

Anele Ngcongca 
Sinethemba Jantjie
Mondli Dlamini
Mondli Cele
Cecil Lolo
Richard Henyekane
Mpho Gift Leremi

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news