Simba SC yamsimamisha Jonas Mkude

Kiungo mkongwe ndani ya Klabu ya Simba kipenzi cha mashabiki, Jonas Mkude amesimamishwa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Taarifa ambayo imetolewa leo na uongozi wa Simba imeeleza kuwa amesimamishwa kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu pamoja na masuala mengine.

Habari hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo imefikia ili kamati ya nidhamu iweze kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zinazomhusu Mkude.

Post a Comment

0 Comments