Hospitali ya Uhuru yaanza kuhudumia wagonjwa wa nje

Hospitali ya Uhuru inayojengwa kwa gharama za sh.bilioni 3.9 imeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje, anaripoti Mwandishi Maalum Diramakini.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Dkt. Dkt.Eusebius Kessy alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo.
Katibu wa Kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma, Meshack Bandawe akizungumza jambo na manesi wanaofanya kazi katika Hospitali ya Uhuru iliyopo Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.Hospitali hiyo ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.8, imeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje. 
Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma, Meshack Bandawe akikagua vifaa mbalimbali vilivyopo katika Hospitali ya Uhuru ambayo imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.

“Hospitali yetu imeanza kutoa huduma tangia tarehe 21 Desemba 2020 na mpaka sasa imeshahudumia wateja takribani 300,”amesema Dkt.Kessy. 

Ameongeza kuwa, ujenzi wa hospitali hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa chamwino na maeneo ya karibu na kusema kuwa watahahakisha kwamba huduma zinakuwa bora kama ilivyokusudiwa. 
Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma, Meshack Bandawe akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Halmshauri ya Wilaya ya Chamwino, Dkt.Eusebius Kessy (kulia) juu ya mashine mbalimbali zilizoletwa hospitali ya uhuru iliyokamilika na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Dodoma.
Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe akipata maelezo mbalimbali juu ya huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Uhuru iliyokamilika na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Dodoma.

Dkt. Kessy amesema kuwa, hospitali hiyo inatoa huduma kwa wagonjwa wenye bima ya afya ya Taifa NHIF na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na pia wale ambao hawana bima ya afya. 

Akizungumzia huduma zinazotolewa kwa sasa, Dkt.Kessy amesema, kwa sasa huduma za maabara,kliniki za macho na meno,mionzi, kliniki za mama na mtoto na huduma za wagonjwa wa nje (OPD). 
Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma, Meshack Bandawe aki akipata maelezo kutoka kwa Mganga mkuu wa halmshauri ya Wilaya ya Chamwino, Dkt.Eusebius Kessy juu ya upatikanaji wa dawa katika chumba cha kuchukulia dawa katika Hospitali ya Uhuru iliyokamilika na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Dodoma. 
Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma, Meshack Bandawe akimjulia hali mgonjwa aliyefika kupata matibabu katika Hospitali ya Uhuru iliyokamilika na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Dodoma. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmshauri ya Wilaya ya Chamwino, Dkt.Eusebius Kessy.

Kwa upande wake Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma, Meshack Bandawe ambae alifanya ziara maalum kukagua maendeleo ya hospitali hiyo amesema kuwa, ujenzi wa hospitali hiyo umekamilika kwa asilimia 99.8. 

Amebainisha kuwa, maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu alipofanya ziara Novemba 20,2020 yametekelezwa ikiwemo kukamilisha ujenzi wa jengo ifikapo tarehe 5 Desemba 2020,vigae vya chini,miundombinu muhimu na ukamilishaji wa ukuta kuzunguka hospitali hiyo ambao umekamilika kwa asilimia 99 na ujenzi wa miundombinu ya barabara hospitalini hapo unaendelea chini ya TARURA na utakamilika hivi karibuni. 

Pamoja na hayo amesema mifumo ya maji na umeme na miundombinu mbalimbali imekamilika pamoja na vifaa tiba vya Utra sound, X-ray,ECG na baadhi ya samani ambavyo vimeshawasili hospitali hapo. 
Jengo la Hospitali ya Uhuru lilikamilika kwa asilimia 99.8 na kugharimu bilioni 3.9 limeanza kutoa huduma kwa wananchi. (Picha zote na MAELEZO). 

Amesema siku ya sherehe za mapinduzi ya Zanzibar kulifanyika uchangiaji wa damu salama na kufanikiwa kupata unit 48 za damu. 

Aidha, amelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia SUMA JKT ambae ndio mkandarasi wa hospitali iyo,mshauri mwelekezi wakala wa majengo Tanzania (TBA), Mkurugenzi wa halmashauri ya Chamwino,Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma na Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa usimamizi wa ujenzi wa hospitali hiyo. 

Lengo la ujenzi wa Hospitali ya Chamwino ni kuboresha huduma za kijamii Dodoma ikiwamo afya ili kutimiza azma ya Serikali kuhamia Dodoma ambayo ndio makao makuu ya nchi. 

Ujenzi wa Hospitali ya Chamwino ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwamba Fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe ya miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania bara za tarehe 9 desemba 2018 zitumike kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Chamwino.

Post a Comment

0 Comments