Mwanachama wa Chama cha Wanaume Wachoyo nchini Sierra Leone aoa kwa kutumia usafiri wa baiskeli

Mmoja wa wanachama wa Chama cha Wanaume Wachoyo nchini Sierra Leone (Sierra Leone Stingy Men Association) ameudhirishia umma kuwa, ukiwa ndani ya Chama unapaswa kuifanyia kazi nara yao kwa vitendo, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Wakiongozwa na nara ya 'subiri nione cha kufanya', mwanachama huyo mkazi wa Makeni ameamua kufunga harusi ya gharama ndogo huku usafiri wao ukiwa ni baiskeli.

"Tuko busy kwa mambo msingi ya kujenga uchumi, ndiyo maana unayaona haya," amekaririwa Bwana harusi huyo, huku akisisitiza kuwa, wamefanya hivyo kupunguza gharama zisizo za msingi kama wanavyoonekana katika picha.
Kwa upande wake, Bibi harusi amekaririwa akisema kuwa, huu ni wakati wa kufanya mambo yasiyo na gharama kwa faida yao.

"Mwanamke mwenye maono, huwa hana bla! bla! nyingi. Wanawake tuwasaidie waume zetu kuokoa mali kwa faida ya watoto wetu,"amekaririwa Bibi harusi.

Chama hiki kimeasisiwa siku za karibuni nchini Nigeria, lakini kwa sasa kinatajwa kushika kasi katika mataifa mbalimbali ya Afrika huku wanachama wengi wakiwa ni vijana na watu mashuhuri wenye ukwasi mkubwa.

Post a Comment

0 Comments